SPORTS & INTERTAINMENTS

MAALIM SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Sharifa Khamis. 




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani 


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar kuwasiliana na Wizara inayohusiana na mambo ya Michezo Tanzania Bara ili kujadiliana juu ya namna ya kutatua changamoto za kimichezo ya kitaifa na kimataifa.

Maalim Seif ametoa agizo hilo baada ya kukutana na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar katika mkutano uliofanyika baraza la wawakilishi la zamani Mnazimmoja, ambapo wadau hao wa michezo walilalamikia ushirikishwaji mdogo wa wanamichezo wa Zanzibar katika michezo inayoiwakilisha Tanzania.

Amesema serikali ina nia thabiti ya kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar ili kuirejeshea sifa yake ya kimichezo iliyokuwa nayo hapo awali.


Wadau hao wa michezo wamesema hadhi ya michezo imeshuka Zanzibar kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo upungufu mkubwa wa viwanja vya michezo hasa ile michezo ya ndani (Indoor games).

Sambamba na hilo wadau hao wa michezo wamesema serikali iliidharau michezo na haikutoa mkazo unaostahiki kuwaendeleza wanamichezo na kuibua vipaji vya wanamichezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Abdillahi Jihadi Hassan amesema tayari Wizara yake imeshaanza mchakato wa kuwasiliana na Wizara ya Elimu Zanzibar wenye lengo la kurejesha michezo maskulini, ambayo itaibua vipaji ambavyo vitaendelezwa na kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar.

Baadhi ya wadau hao wameiomba serikali kutodharau michezo ya asili ikiwemo mchezo wa karata, mchezo wa ng’ombe na kuogelea ambayo inaendana na utamaduni wa Zanzibar na husaidia pia shughuli za utalii




 ROONEY KAMA BECKHAM; MKEWE ATANGAZA JINSIA YA MTOTO WAO ANAYETARAJIWA KUZALIWA MAY 2013


Tayari wameshafanikiwa kuwa na mtoto wa kiume katika familia yao, lakini kama vile haitoshi Collen na Wayne Rooney wanategemea kumkaribisha dume lingine katika familia yao hvi karibuni.

Coolen, 27, ambaye ni mjamzito wa mtoto wake wa pili, alitangaza jinsia ya mtoto wake aliye tumboni kwenye mtandao wa kijamii wa Twiter na akasema mshambuliaji wa United, Rooney amezipokea taarifa hizo kwa furaha kubwa.

Aliandika hivi kwenye akaunti yake ya Twiiter

Coleen na Wayne tayari ni wazazi wa Kai, na sasa wanategemea kuongeza kidume kingine ndani ya nyumba mnamo mwezi wa tano mwakani. 



 MKE WA SNEIJDER ASEMA''TUNAONDOKA MILAN MWEZI JANUARY''


Mke wa Wesley Sneijder amesema kwamba mumewe ataondoka Inter wakati dirisha la usajili la mwezi January.

"Tunakaribia kuondoka Milan," Yolanthe Cabau aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi. "Kila kitakuwa kimewekwa vizuri katika siku za mwanzo za mwezi January.

"Tutakapohamia? Tunaangalia mahala pazuri kwa ajili ya familia yetu. Kwa sasa hivi sijali sana kuhsu kazi yangu."

Sneijder amekuwa kwenye kutokuelewana na Inter katika siku za hivi karibuni baada ya kukataa ombi lao kwa mchezaji apunguze kiasi cha €2m kutoka kwenye mshahara wake.

Hajaichezea timu hiyo ya Serie A tangu alipocheza dhidi Chievo, kwanza kwa sababu ya majeruhi na baadae kwa sababu za kiufundi za boss Andrea Stramaccioni.

Sneijder aliruhusiwa kuanza mapumziko yake ya Christmas mapema wiki hii pamoja na kwamba Inter bado wana mechi mbili  za kucheza


 YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA AFRICA TUZO ZA CAF-AWAFUNIKA DROBBA, NA ETO'O-ABOUTRIKA MCHEZAJI BORA NDANI YA AFRICA-ZAMBIA KIBOKO YAO


Kiungo wa Ivory Coast  na Manchester City Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya pili mfululizo usiku wa Alhamisi, akimshinda mmpizani wake wa karibu Didier Drogba 

Kiungo huyo mwenye miaka 29 ambaye katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, alichangia kwa kiasi kikubwa kuisadia Ivory Coast kucheza fainali ya AFCON 2012 pai alikuwa ndio mhimili wa Manchester City mpaka walipochukua ubingwa wa England mwezi June mwaka huu.

Pia alikuwa mmoja wa wafungaji katika mechi ya ushindi wa kombe la hisani dhidi ya Chelsea ambapo City walishinda kwa 3-2 - huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2013.

Didier Drogba alishika nafasi ya pili, huku kiungo wa Barcelona Alexander Song akikamata nafasi ya 3 katika tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra usiku wa kuamkia leo.

Mohamed Aboutrika alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara, huku timu yake ya Al Ahly ikichaguliwa kuwa timu bora kwa upande wa vilabu wakati mabingwa wa Afrika kitaifa Zambia wakichaguliwa timu bora ya taifa. Tuzo zilikuwa kama ifuatavyo

CAF AWARDS
Player of the Year - Yaya Toure
African based Player of the Year - Mohammed Aboutrika
Women's Footballer of the Year - Genoveva Anonma (Equatorial Guinea)
National team of the Year - Zambia
Coach of the Year - Herve Renard (Zambia)
Club of the Year - Al Ahly
Legends Award: Mahmoud El Gohary (Egypt) and Rigobert Song (Cameroon)
National Women's Team of the Year - Equatorial Guinea
Fair Play Award - Gabon national team supporters
Most Promising talent of the Year - Mohamed Salah (Egypt and FC Basel) 




HIVI NDIVYO TUZO YA BALLON D'OR INAVYOTENGENEZWA - RONALDO, MESSI, AU INIESTA NANI KUIBUKA KIDEDEA WIKI 2 ZIJAZO????

RONALDO, INIESTA OR MESSSI

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Timu ya masonara sita ndio wanashughulikia utengenezwaji wa tuzo ya Ballon d'Or

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Utengenezaji wa Ballon d'Or ukiendelea

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Ufaransa ndio imekuwa nchi inayotengeneza tuzo tangu mwaka 1956.


Piece by piece: The same family-run store in Paris have built the trophy every year since 1956
Mtengenezaji akiweka kipande kimojawapo kwenye tuzo hiyo

Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?
Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?

No comments:

Post a Comment