Friday, January 4, 2013

MASTAA BONGO MOVIE WASEMA YAO YA MOYONI KUHUSU KIFO CHA SAJUKI!


LIBERT MSUYA STAA WA FILAMU YA HOUSE BOY:" Haitosahaulika kwa historia ya sanaa ya filmua Tanzania ni miaka miwili tu tumeondokewa na wapiganaji wenzetu ambao tulikuwa bado tunawapenda na kushirikiana nao kwa kila jambo kuhusu sanaa yetu.Lakini Mungu ameonesha upendo zaidi kwao na amewatwa.Tunawatakia mapumziko mema ya milele Ameen"
  MZEE MAGALI:" Sasa ni wakati wa kuyakabidhi maisha yetu kwa bwana hakika maisha yamekuwa mafupi sana wanaondoka vijana wadogo ambao ni nguvu kazi ya taifa. Lakini kazi ya mungu haina makosa"
NISHA" Jamani sijui ni nini? kweli binadamu tunapaswa kukesha katika maombi maana miaka hii miwili wameondoka ndugu zetu mfululizo...Lakini kazi ya muumba haina makosa tuwaombee wapumnziko mahali pema peponi kwa vile wao wametangulia sisi tupo nyuma yao" Amina
 WEMA SEPETU: "Kwa kweli hadi inaogopesha licha ya kuwa sisi binadamu kufa ni lazima lakini inaumiza kuona vijana wenzetu wanaondoka mapema,Upande mwingine nafahamu kila kitu hupangwa na mungu hivyo kazi yake haina makosa jina lake lihimidiwe Ameeen"

 ELIYA DEVID MJATA:"Kazi ya Mungu haina makosa Sajuki tulimpenda sana ndio maana wasanii,watanzania tuliungana kufanya jitihada za kunusuru maisha yake kwa kujitolea kwa michango mbalimbali lakini  mwisho wa siku baba Mungu hakupenda. Kapumnzike kwa amani mdogo wangu" Ameen
 BAMBO:"Nilimfahamu Sajuki tangu Kaole ambapo alikuwa msanii mwenye ndoto za mafanikio lakini kutokana na mapenzi yake aliyetuumba ametutoka na kazi yake imeisha hapo kiimani. Hivyo kazi imebaki kwetu sisi tulibaki hai tunajiandaaje na safari?  Bwana ametoa na sasa ametwaa jina lake lihimidiwe milele Ameen"
 J.WOLPER:"Kwa kweli kifo cha Sajuki kimetacha kwenye wakati mgumu sio kwenye familia yake tu bali ni kwa sisi thote tulimpenda sana lakini mungu amempenda zaini tumuombee aipumnzishe roho yake mahali pema peponi Ameen "
MANAIKI SANGa mwanamuziki na muigizaji:" Rest In Peace Bro tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda sana, thote tuko njia hiyo hiyo mbele yetu nyuma yako"

No comments:

Post a Comment