Wednesday, January 2, 2013

TUNALAANI SANA UNYAMA HUU;INASIKITISHA SANA JINSI BINTI HUYU ALIVYO BAKWA HADI KUFA

 Huyu ndiye binti aliyebakwa hadi kufa nchini India
         New Daily India

HIVYO ndivyo binti wa miaka 23 aliyekuwa mwanafunzi alivyobakwa na wakatili nchini India hadi kufa. Binti huyo alifariki dunia na mwili wake kuchomwa moto kama ilivyo mila na desturi za wahindi wakabila la Baniani na waumini wa dini ya Baniani.
Binti huyo alikutana na unyama huo wakati alipokuwa akitoka kumtembelea rafiki yake wakiume, nakukutana wakatili hao baada ya kukosea kupanda basi ambalo halikuwa la abiria.
Katika gari hilo lililokuwa na wanaume sita alijikuta akiwa msichana pekee ndani ya basi hilo. Wanaume hao waliamua kumfanyia binti huyo mdogo ukatili wa kutisha baada ya kubakwa na kila mwanaume ndani ya gari hilo.
Hata hivyo baada ya wanaume hao kufanikiwa kumbaka binti huyo, waliaamua kutoboa sehemu zake za siri pamoja kutoboa utumbo wake mpana na mwembamba kwatumia vyuma vinavya onyesha alama za barabrani wakiwa na lengo la kumuuwa ili wapoteze ushahidi.
Hata hivyo baada ya unyama huo wakatili hao walimtupa pembeni mwa barabara akiwa uchi wa mnyaka huku wakijua kuwa kafa na hatimaye wakatokea kusiko julikana. Ingawa Mungu amemchukuwa bint huyo mdogo asiyekuwa na hatia katika maisha yake na kukatishwa ndoto zabaaye.
Nakulingana na unyama aliofanyiwa binti huyo mdogo,watalaam wanasema kwamba asingeweza kufurahia maisha yake ya ndoa na kabla ya kufa kwake alikuwa akishinda akitokwa machozi,na kuzimia mara tano kwa siku. Pamoja na kwamba binti huyo ameshazikwa, lakini  Habarimpya.com inaungana na na watu wote duniani walioguswa na unyama aliofanyiwa binti huyo.
Bila kujali kwamba hakuwa ndugu yako,hakuwa rafiki yako wala hakuwa mwanao,dada yako ama mdogo wako ungana na gfrankson.blogspot.com kulaani unyama huo kwa ku-share ,ku-like na kutoa maoni yako chini ya habari hii, ili ujumbe huu wa kupiga vita dhidi ya ukatili uzidi kuenea duniani kote. Kwani unyama kama huu unaweza kukutokea hata wewe unayesoma makala haya popote ulipo,ama mwanao,ndugu,yako mkeo mpenzi wako rafiki yako ama mdogo gfrankson.blogspot.com  itawaletea mfululizo wa maisha ya ukatili nchini india, endeleeni kufuatlia mikasa ya kutisha nchini humo

No comments:

Post a Comment