Friday, September 6, 2013

EXCLUSIVE: LADY JAYDEE KUTOA AJIRA KWA LULU NYUMBANI LOUNGE. ISHU YENYEWE ITAKUA HIVI........

Elizabeth Michael, Judth Wambura
Lady Jay D Lulu wanatarajia kufanya onyesho la kufa mtu nyumbani Lounge.
BAADA ya kufanya vizuri katika uzinduzi wa filamu yake mwanadada Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonekana kumvutia sana mwanamuziki Judth Wambura ‘Lady Laydee’ na kuamua kuandaa Onyesho litalaowakutanisha pamoja na kuimba katika jukwaa moja na kuimba wimbo maalum wa Yahaya.

.
Elizabeth Michael
Lulu mwigizaji wa filamu sasa anaingia katika muziki.
Judith Wambura
Lady Jaydee mwanamuziki mahiri Bongo Ijumaa hii atawasha moto akiwa na Lulu Nyumbani Lounge.
Ladies Nite
Show ya nguvu kuangushwa Nyumbani Lounge
Lulu siku ya uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age aliweza kuwashangaza waarikwa waliohudhuria show baada ya kuimba wimbo wa Yahaya sambamba na Anaconda na kushangiliwa na umati wa wapenzi wa filamu wanakutana tena na kuimba kwa mara nyingine.
Lady Jaydee na Machozi Band wakishirikiana na msanii mwarikwa Lulu watafanya bonge show kesho siku ya Ijumaa katika viwanja tulivu vya Nyumbani Lounge ni show ya Ladies Nite nyote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment