Thursday, February 7, 2013

MELI YA MV VICTORIA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO.


MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo. Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka. Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.

No comments:

Post a Comment