MAALIM SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao
ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani. Kulia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo Zanzibar, Sharifa Khamis.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na
viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar, kwenye mkutano na wadau hao
ulifanyika Baraza la Wawakilishi la zamani
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameiagiza
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar kuwasiliana na
Wizara inayohusiana na mambo ya Michezo Tanzania Bara ili kujadiliana
juu ya namna ya kutatua changamoto za kimichezo ya kitaifa na
kimataifa.
Maalim
Seif ametoa agizo hilo baada ya kukutana na viongozi wa vyama vya
michezo Zanzibar katika mkutano uliofanyika baraza la wawakilishi la
zamani Mnazimmoja, ambapo wadau hao wa michezo walilalamikia
ushirikishwaji mdogo wa wanamichezo wa Zanzibar katika michezo
inayoiwakilisha Tanzania.
Amesema
serikali ina nia thabiti ya kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar ili
kuirejeshea sifa yake ya kimichezo iliyokuwa nayo hapo awali.
Wadau
hao wa michezo wamesema hadhi ya michezo imeshuka Zanzibar kutokana na
sababu mbali mbali zikiwemo upungufu mkubwa wa viwanja vya michezo
hasa ile michezo ya ndani (Indoor games).
Sambamba
na hilo wadau hao wa michezo wamesema serikali iliidharau michezo na
haikutoa mkazo unaostahiki kuwaendeleza wanamichezo na kuibua vipaji
vya wanamichezo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Abdillahi Jihadi
Hassan amesema tayari Wizara yake imeshaanza mchakato wa kuwasiliana na
Wizara ya Elimu Zanzibar wenye lengo la kurejesha michezo maskulini,
ambayo itaibua vipaji ambavyo vitaendelezwa na kurejesha hadhi ya
michezo Zanzibar.
ROONEY KAMA BECKHAM; MKEWE ATANGAZA JINSIA YA MTOTO WAO ANAYETARAJIWA KUZALIWA MAY 2013
Coolen, 27, ambaye ni mjamzito wa mtoto wake wa pili, alitangaza jinsia ya mtoto wake aliye tumboni kwenye mtandao wa kijamii wa Twiter na akasema mshambuliaji wa United, Rooney amezipokea taarifa hizo kwa furaha kubwa.
Aliandika hivi kwenye akaunti yake ya Twiiter
Coleen na Wayne tayari ni wazazi wa Kai, na sasa wanategemea kuongeza kidume kingine ndani ya nyumba mnamo mwezi wa tano mwakani.
MKE WA SNEIJDER ASEMA''TUNAONDOKA MILAN MWEZI JANUARY''
"Tunakaribia kuondoka Milan," Yolanthe Cabau aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi. "Kila kitakuwa kimewekwa vizuri katika siku za mwanzo za mwezi January.
"Tutakapohamia? Tunaangalia mahala pazuri kwa ajili ya familia yetu. Kwa sasa hivi sijali sana kuhsu kazi yangu."
Sneijder amekuwa kwenye kutokuelewana na Inter katika siku za hivi karibuni baada ya kukataa ombi lao kwa mchezaji apunguze kiasi cha €2m kutoka kwenye mshahara wake.
Hajaichezea timu hiyo ya Serie A tangu alipocheza dhidi Chievo, kwanza kwa sababu ya majeruhi na baadae kwa sababu za kiufundi za boss Andrea Stramaccioni.
Sneijder aliruhusiwa kuanza mapumziko yake ya Christmas mapema wiki hii pamoja na kwamba Inter bado wana mechi mbili za kucheza
YAYA TOURE MCHEZAJI BORA WA AFRICA TUZO ZA CAF-AWAFUNIKA DROBBA, NA ETO'O-ABOUTRIKA MCHEZAJI BORA NDANI YA AFRICA-ZAMBIA KIBOKO YAO
Kiungo huyo mwenye miaka 29 ambaye katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, alichangia kwa kiasi kikubwa kuisadia Ivory Coast kucheza fainali ya AFCON 2012 pai alikuwa ndio mhimili wa Manchester City mpaka walipochukua ubingwa wa England mwezi June mwaka huu.
Pia alikuwa mmoja wa wafungaji katika mechi ya ushindi wa kombe la hisani dhidi ya Chelsea ambapo City walishinda kwa 3-2 - huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2013.
Didier Drogba alishika nafasi ya pili, huku kiungo wa Barcelona Alexander Song akikamata nafasi ya 3 katika tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra usiku wa kuamkia leo.
Mohamed Aboutrika alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara, huku timu yake ya Al Ahly ikichaguliwa kuwa timu bora kwa upande wa vilabu wakati mabingwa wa Afrika kitaifa Zambia wakichaguliwa timu bora ya taifa. Tuzo zilikuwa kama ifuatavyo
CAF AWARDS
Player of the Year - Yaya Toure
African based Player of the Year - Mohammed Aboutrika
Women's Footballer of the Year - Genoveva Anonma (Equatorial Guinea)
National team of the Year - Zambia
Coach of the Year - Herve Renard (Zambia)
Club of the Year - Al Ahly
Legends Award: Mahmoud El Gohary (Egypt) and Rigobert Song (Cameroon)
National Women's Team of the Year - Equatorial Guinea
Fair Play Award - Gabon national team supporters
Most Promising talent of the Year - Mohamed Salah (Egypt and FC Basel)
HIVI NDIVYO TUZO YA BALLON D'OR INAVYOTENGENEZWA - RONALDO, MESSI, AU INIESTA NANI KUIBUKA KIDEDEA WIKI 2 ZIJAZO????
Timu ya masonara sita ndio wanashughulikia utengenezwaji wa tuzo ya Ballon d'Or
Utengenezaji wa Ballon d'Or ukiendelea |
Mtengenezaji akiweka kipande kimojawapo kwenye tuzo hiyo |
No comments:
Post a Comment