Thursday, February 7, 2013

PICHA ZA NGONO TANZANIA ZINAHAMASISHWA NA MASTAA WA BONGO?.

 Kadri siku zinavyozidi kwenda vinaibuka vyanzo kibao vinavyosababisha kushamiri kwa ngono za wazi mbele ya maelfu ya wananchini wa Tanzania.


Gazeti moja la Global Publishers lilimtoa msanii wa Bongo flava BABY MADAHA akionekana jukwaani akiwa ameachia matiti yake nje... tizama picha hizi zilizotokea kwenye gazeti....

Hivi ndivyo alivyoonekana.
Kipindi kifupi kilichopita kupitia magazeti ya Global Publishers tuliona katika ukurasa wa mbele ukionyesha picha za waigizaji maarufu wa filamu hapa Tanzania yani "Wema Sepetu na Aunt Ezekiel" wakiwa wameacha sehemu zao za siri nje nje.

Hizi nafuu hawakuwa uchi kiivyo lakini...nyingine.....

Lakini kutokana na watanzania kutovumilia na kutozoea kuona mambo hayo hadharani, vyombo vya habari pamoja na wananchi walianza kunong'ona wazi wazi, kitu ambacho kiliwafanya mastaa hao wajihisi aibu na kuamua kuwaita waandishi wa habari na kuwaomba watanzania msamaha kuwa hawatorudia kuvaa vile.

Aunt Ezekiel akiomba msamaha kwa watanzania kupitia habari maelezo na waandishi wa habari.

Wema nae alifanya hivyo hivyo..kuomba msamaha kwa watanzania kuwa hatorudia kuvaa nusu utupu.
Ukitupilia mbali skendo za baadhi ya wasanii wa filamu wa zamani waliokuwa wauzaji wazuri wa magazeti ya udaku kama NORA na SINTA na wengine ambao ndio walifungua wigo wa kung'ara katika sanaa kwa kuandikwa vibaya, sasa wanaong'ara kwa sasa ni aibu tupu.

Nimekuwa nikifuatilia magazeti kwa ukaribu sana, baada ya sakata la Wema na Aunt Ezekiel kufifia liliibuka lingine japokuwa halikushika chati sana lakini ni moja ya njia ya uhamasishaji wa ngono Tanzania.

Kupitia gazeti moja la Global Publisher lilitoa picha za muimbaji wa muziki wa mduara nchini ..SHILOLE akionekana jukwaani akiwa hajavaa nguo za ndani, mapozi aliyokuwa akiwawekea watanzania walitosheka....labda huenda huo mtindo huo ukawa ni asili ya mduara, lakini kama ninavyojua asili ya mduara sio kutovaa nguo za ndani tena hadharani!!!

Achana na SHILOLE tuhamie BONGO MOVIE huku siwezi kusema saana kwasababu wengi wetu movie za kibongo tunaziona kwa wingi... yataka moyo nyingi zao kuzitizama kama familia nzima yani Baba, Mama, kaka na dada ni nuksi tupu. Nawapongeza sana wacheza filamu na maigizo... Mhogo Mchungu, Dokta Cheni, JB, Ray, Pembe, Bambo, Kingwendu, Swebe, Seki,Joti na Mpoki, Steven Kanumba Mungu amlaze mahali pema peponi kwa kuitangaza sanaa ya filamu nje ya Tanzania na wengine kibao niliowaacha, kwani nkiwataja sitawamaliza leo. Mengi Nay wa mitego ameyagusia japokuwa ujumbe wa Nay hauwagusi wote bali baadhi yao.


Kupitia gazeti la AMANI la na mengine mengi yaliyokuwa yakitoa picha za UFUSKA za jiji la Dar es salaam, lilitoa picha za wadada warembo safi kabisa wanaojiuza.. lakini kibaya zaidi waliweka hadi viwango vya fedha wanazowatoza wateja wao baada ya kufanya mapenzi.

AMANI




No comments:

Post a Comment