Wednesday, December 26, 2012

# FAHAMU KUHUSU JAFFARHYMES KUKATA TAMAA YA KUMDAKA MWIZI WA VIFAA VYA GARI YAKE.#



Baada ya kupigwa vifaa vya gari yake ikiwepo power windows  zenye thamani ya jumla ikiwa ni shilingi laki nane za kiTanzania, msanii Jaffarhymes ambaye amekuwa katika mishe mishe za kuvisaka kwa wale madaktari wa haya mambo hapa town, ameamua kukata tamaa na kusitisha zoezi hilo.

Jaffarymes amesema kuwa kwa sasa ameamua kujipiga na kununua vifaa hivyo ili aweze kuendelea kutumia gari lake hilo aina ya Harrier katika mishe mishe zake za kila siku kutokana na kulipaki muda wote akiwa anasubiria uwezekano wa kupata mali zake.
Itakumbukwa kuwa msanii huyu alipatwa na maswahiba haya huko mitaa ya Kijitonyama ambapo ndipo kwao siku ya Ijumaa, na hadi kufikia leo na siku zinazoendelea, matumaini ya kumdaka mwizi ndiyo yamekuwa yakizidi kuyoyoma.

No comments:

Post a Comment