Polisi
nchini Uganda wameanza msako wa watengenezaji wa pombe ya kienyeji aina
ya gin, iliyosababisha vifo vya watu wanne na kuwasababishia upofu
wengine wawili ndani ya wiki mbili.Polisi
wamesema watu hao walikufa baada ya kunywa pombe hiyo kwenye baa
inayomilikiwa na watengenezaji pombe kwenye makazi duni ya vitongoji
vya Katanga, Kikumikikumi karibu na Makerere na kitongoji cha Sir
Apollo Kaggwa Jijini Kampla.
Mkuu
wa Polisi wa Kituo cha Wandegeya, Ceasar Tusingwire amesema wanadhani
kuwa watu hao walikufa baada ya kunywa pombe hiyo iliyokuwa imefungwa
kwenye vifungashio vya mifuko ya plastiki na kwenye madumu.
Kufuatia
tukio hilo polisi nchini Uganda imewaonya wananchi kutopendelea
kunywa pombe za kienyeji kutokana na nyingi kuwa na dalili za sumu.
No comments:
Post a Comment