Takribani
watu 128 wamekufa nchini Urusi kutokana na baridi kali huku wengine
2,000 wakilazimika kutafuta huduma za matibabu wengi wao kutokana na
kufa ganzi na kuganda damu mwilini.
Wengi wa waathiriwa wamesemekana kuwa watu wasiokuwa na makaazi.
Mjini Moscow, viwango vya joto vimepungua hadi nyuzijoto 32 chini ya sifuri.
Mashariki
ya Siberia nyuzi joto zimefikia alama ya 60 chini ya sifuri, hata hivyo
watabiri wa hali ya hewa wamesema hali inatarajiwa kubadilika katika
eneo la katikati ya Ulaya la Urusi, ikiwa ni pamoja na Moscow baadaye
wiki hii.
No comments:
Post a Comment