KUTOKANA na bifu linalofukuta kama moto wa kifuu kati ya waigizaji, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameibuka na kumchana Shilole kuwa analitamani Gereza la Segerea. Akichonga na paparazi wetu, Baby Madaha ‘aliyelinunua’ sakata hilo, alimtaka Shilole kuacha kumfuatafuata shosti wake (Flora) kwani yeye hana lolote zaidi ya kuropoka maneno machafu. “Eti Shilole anatangaza kuwa atanipiga mimi hebu ajaribu kama yeye mwanamke kweli, mimi haniwezi kamwe. Kwanza hajielewi hata thamani yake, kutwa kutembea na watoto wadogo halafu anajiona staa,” alisema Baby Madaha |
Monday, January 21, 2013
BABY MADAHA ATISHIA KUMUWEKA SHILOLE RUMANDE..!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment