Tuesday, January 29, 2013

DONDOO MUHIMU KUHUSU KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU KILICHOENDESHWA NA WAZIRI MKUU HUKO MTWARA



Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013
------------------
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.

Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
 Taarifa mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.


UPDATES/TAARIFA MPYA za ziara ya Waziri Mkuu Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.

Dondoo muhimu:

  • Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
  • Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
  • Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
  • Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
  • Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
  • Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
  • Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
  • Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
  • Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu

No comments:

Post a Comment