Monday, January 7, 2013

FAHAMU KUHUSU KUNDI LA PA 1 KUVUNJIKA NA SABABU.


Rapper na Producer wa Kundi la Pa 1 `Nah Real' amekaririwa na sammisago.com Leo 10:00 Am, 7 Jan 2012 akisema hawezi kuthibitisha kwamba kundi hilo limevunjika ila kwa sasa hawana maelewano mazuri ndani ya kundi na kazi za Pa 1 zimesimamishwa kwa sasa.Yeye kama msanii hawezi kusema Kundi limevunjika mpaka Management ya Kundi itoe tamko. Pia Nah Real amekata kutaja sababu za kutokuelewana ndani ya kundi la Pa 1 sababu hizo zinaweza kurekebishwa.
Pah One
Awali ilisemekana kuwa mahusiano ya Nah Real na Aika kuvunjika ndio chanzo cha kundi kuyumba ila Nah Real amesema hajagombana na Girl Friend wake Aika ambaye ni member wa Kundi Hili na wao na mahusianio yao hayahusiki na mambo ya kundi. So Story za wao kugombana ndio maana kundi linayumba sio za Kweli na yeye na Aika Bado wapo pamoja. Tunasubiri tamko la Utawala wa Pa 1.

No comments:

Post a Comment