![]() |
Vanessa |
Sauti ya Vanessa Mdee ni mpya katika anga la muziki
Tanzania, kwangu mimi ni ushahidi mwingine kuwa kipaji huwa kinatembea katika
familia. Kwa kweli kilichonifanya nitake kusikiliza muziki wa huyu binti ni jina hili la Mdee. Mwaka 1972
nilijiunga na Chuo cha Ualimu
Kleruu Iringa, pale chuoni kulikuwa na magitaa mapya kabisa, hiyo
ilisababisha wote tuliokuwa wapiga magitaa kujenga urafiki na kukusanyika kila
jioni kwenye kachumba kadogo na
kufanya mazoezi, kwa kuwa chuo kilikuwa tayari kina mwaka mmoja tulikuta
tayari
wananchuo waliotangulia walikuwa wameanzisha bendi, na hapo ndipo
nikamuona kwa
mara ya kwanza mtengeneza filamu mashuhuri kutoka Tanga Kassim El Siagi
akiwa
anapiga gitaa la solo. Kati ya wanachuo tulioingia mwaka huo pia
alikuweko
mmoja aliyeitwa Yusuph Mdee. Tulipatana mara moja baada ya kujiona wote
tunapenda muziki aina moja, haraka tukafanya mpango mpaka kuweza kuishi
katika chumba kimoja na magitaa yetu, tulipenda kupiga na kuimba muziki
uliokuwa maarufu
wakati huo, muziki wa soul, uliokuwa ukitamba wakati huo na wanamuziki
kama
Otis Redding, James Brown, Percy Sledge, Clarence Carter na wengine
wengi. Na
pia tulipenda muziki wa bendi wa bendi za Kitanzania zilizokuwa zikipiga
muziki
wenye uhusiano na huo, kama Afro70, Safari Trippers, Sparks, Commets na
kadhalika. Yusuph alikuwa wakati huo ametoka Dar es salaam ambapo aliwa
mwanamuziki
mzuri wa bendi maarufu ya Upanga iliyokuwa ikiitwa the Groove Makers,
ambayo
ilikuwa na wanamuziki maarufu
ambao kwa sasa wana nyadhifa nzito serikalini, hivyo sitawataja
hapa, lakini sisi tukawa katika mpango
wa kujaribu kupiga muziki tulioupenda . Yusuph alikuwa muimbaji na
mpigaji
mzuri wa gitaa, baadae alijikita zaidi katika uchoraji na hata kufikia
kwenda
Italy kuendeleza fani yake hiyo, aliishi Arusha kwa muda mrefu akiwa
graphic
artist na DJ maarufu wa wakati wake, urafiki wetu ulidumu mpaka
alipofariki Oktober 1999. Kwa kuufahamu uhusiano wa Vanessa na Yusuph
nayaona mambo mengi ya Yusuph katika Vanessa japo sidhani kama Vanesa
anaona hivyo kutokana na tofauti kubwa ya umri kati ya Yusuph na
Vanessa. Uhakika nilionao ni kuwa ikiwa Vanessa ataendelea na ubora
alionao sasa ni wazi akiwa na menejment nzuri atafika mbali sana. Wish
you all the best Vanessa
No comments:
Post a Comment