Tuesday, January 1, 2013

KAULI YA WASTARA AKIPINGA KUMFANYA SAJUKI CHANZO CHA KUJIPATIA PESA




MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo, Wastara Juma 'Stara', amesema katika maisha yake amegundua kuwa kuingia katika fani ya uigizaji kumemfanya afilisike tofauti alivyokuwa awali akifanya shughuli zake za biashara.

Msanii huyo alifikia kusema hayo kwa uchungu baada ya baadhi ya wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Unity kudai kuwa msanii huyo amemfanya Sajuki (mumewe am ambaye pia ni msanii) mtaji wa kujipatia fedha.
Mtu asiyekujua anaweza kukutukana kwa kukupa jina lolote ili aweze kufurahisha nafsi yake, nimeumia sana kusikia kuwa mume wangu ana fedha lakini mimi nimemgeuza Sajuki kitega uchumi kwa kuomba misaada kwa watu," alisema.

"Mimi si mtu wa namna hiyo na sijalelewa katika maisha ya kimasikini, nilikuwa najua kuwa hao Bongo Movie ni ndugu zangu na kupokea ushauri wao, lakini nimejifunza kutoka kwao kuwa mwanadamu anaweza kukuchekea mdomoni lakini akakusimanga moyoni."

Stara akiongea kwa huzuni amedai kuwa alipoandaa tamasha la Asante Tanzania mkoani Arusha, ndipo vituko vilipoanza kwa wasanii aliopanga nao kufanya tamasha hilo kubadilika na kufanya tamasha lao mjini humo siku moja kabla ya lile walilopanga.

Anasema wasanii hao walifanya hivyo kwa maelezo kuwa katika tamasha lililotangulia mjini Iringa, waligundua kuwa Sajuki ana fedha kutokana na namna walivyoandaliwa sehemu nzuri ya kulala na kulishwa vizuri pia.

Hata hivyo mwanadada huyo anawashukuru watu kwa misaada yao huku akimwachia Mungu akiamini kuwa kila jambo ni mapito.

Kwa sasa Sajuki ambaye amekuwa mgonjwa kwa muda, amelazwa tena hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kubadilika. Yuko chini ya uangalizi wa madaktari akisubiri kurudishwa India kwa matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment