MUIGIZAJI wa siku nyingi Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’,
amedai kuwa maisha yake ni ya kawaida na haishi kwa kujiumiza kichwa
kwani kile anachokipata kinamtosha na hajawahi kutumia njia za mkato
kupata mali kama wengine wanavyofanya, kwa kujiuza kwenye hoteli kubwa
kubwa ili tu wapate wanaume wenye pesa nyingi.
Wakati alipozungumzia juu ya wasanii wanaojiunza kwenye hoteli kubwa kubwa, mwandishi wa mtandao wa DarTalk alitaka
kujua kiundani ishu hiyo, ndipo alipodai kuwa wapo baadhi ya
nyota wanaofanya kazi hiyo kwa kuwa hawaithamini miili yao na ndiyo
maana wanafanya hivyo.
Akiongea na DarTalk, Shumileta alidai
kuwa uwepo wake kwenye game kwa muda mrefu kumemfanya ajifunze mambo
mengi na huwa anashika kichwa pale anapowaona wasanii waliokuja juzi
kwenye tasnia hiyo wakijiona kama wakongwe wakati hakuna kitu
wanachokijua.
Alisema
kuwa yapo mabaya mengi anayoyajua lakini wasanii wengine anapowaelekeza
wamekuwa wajuaji sana hivyo anawaacha na anawachukulia kama wao
wanavyotaka, lakini wengi wanapotea kutokana na kutojua wanatakiwa
waishi vipi ili kwenda sawa na umaarufu walionao.
“Ukubwa
dawa unajua kuna wasanii wamekuja jana lakini wanashindwa kuelewa
kwamba yule uliyemkuta lazima umpe heshima yake wao hawajui hilo, kwa
sababu tu wanafanya vizuri majina yanajulikana basi, lakini kuna mambo
ambayo wanafanya wanapotea na watu kama sisi tunayajua lakini
tunashindwa kuwaambia kwa sababu wanakauli za kuudhi,” alisema.
No comments:
Post a Comment