DAR ES SALAAM,
Tanzania
Naye Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia (DP), Christopher Mtikila, amemtaka Rais Kikwete kutumia hekima
katika kumaliza mgogoro wa gesi na maslahi ya Mtwara kinyume chake nchi inaweza
kugawanyika.
Akizungumza na wandishi wa
habari Dar es Salaam leo, Mtikila alisema kuwa madai ya kwamba umeme wa gesi
hiyo ufuliwe kulekule Kusini yanatokana na uchungu wa wananchi wote wa
Kusini.
Alisema iwapo moto wa mgogoro
huo hatauzimwa kwa hekima si ajabu ukaimeza mikoa yote ya Kusini ikiwemo Lindi,
Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro na hata Rukwa
ambapo matokeo yake kuzaliwa mataifa mawili mpaka ukiwa reli ya
kati.
Mtikila alisema wakazi wa
kusini hawazuii gesi hiyo isitoke bali wanachotaka umeme huo ufuliwe kule kule,
lengo likiwa ni kuwaletea mapinduzi ya maendeleo.
“Wananchi wa Mtwara
wanafahamu kwamba sumaku ya mandeleo ya uwekezaji wa miradi mikubwa ya kuwaletea
maendeleo ni nishati na miundombinu, lakini watawala wa CCM waliwanyang’anya
reli ya kusini kwa uharamia wa kung’oa mpaka mataruma na kufutilia mbali hata na
tuta lenyewe,”alisema.
Aliongeza kuwa Rais Kikwete
analazimika pia kutamka bayana kipaumbele kwa uboreshaji wa Bandari Kuu ya
Mwara, ikibidi hata kwa kusitisha mradi wa Bandari ya
Bagamoyo.
Kwamba njia pkee ya kuzima
moto huo kusini na kurejesha amani ni Rais huyo kutoa tamko la kukubali
kufuliwa umeme huo mkoani Mtwara kwa ajili ya maslahi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment