Tuesday, January 1, 2013

"NATAMANI KUOKOKA NA KUANZA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI"...JINI KABULA



 MSANII wa filamu na muziki Bongo Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ anasema kuwa muziki anaofanya na kundi lake la Scopion Girls ni wa muda tu kama anafanya mazoezi, anafanya hivyo kwa sababu mara nyingi makundi ya muziki wa kizazi kipya hayadumu kwa mantiki hiyo iwapo kundi lao litakufa ataingia rasmi katika kuimba muziki wa Injili.

“Nafanya muziki nikiwa na kundi lengo ni kudumu kwa muda mrefu lakini kama itatokea kuvunjika kundi langu la Scopion Girls basi nitaimba nikiwa pekee yangu lakini si muziki huu wa kidunia bali nitamwimbia Mungu wangu kwa kuimba muziki wa Injili kwa sababu  natamani sanakuokoka,”anasema Jini Kabula.


jini kabula  akipigana denda  na jack
 
Jini Kabula ambaye ni mzazi mwenzake na mwigizaji na mkurugenzi wa Tuesday Entertainment Ltd Mr. Chuzi pamoja na kuimba muziki pia ni mwigizaji nyota aliyejichukulia umaarufu katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu na kushiriki katika filamu nyingi zinazoandaliwa na kampuni mbalimbali.

No comments:

Post a Comment