Rapper kutoka MLab, Nikki Mbishi hivi karibuni alimpa rapper mwenzie Stamina, ubunge wa Morogoro kwa kumfananisha na Mh. Joseph Mbilinyi [SUGU] kwa kazi nzuri anayofanya kuuwakilisha mkoa huo kimuziki. Nikki Mbishi aliyasema haya hasa kwa kuonekana kukubali anachofanya Stamina kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, na kuandika "Stamina is our new SUGU, mbunge wa Morogoro".
Hii ni heshima kubwa sana aliyompa Stamina hasa kwa kumfananisha na SUGU, hasa ukizingatia Nikki Mbishi ni msanii mkubwa kuliko Stamina. Hii inaonesha ni jinsi gani Nikki Mbishi anamkubali rapper huyu from Moro Town.
Well hii ni nzuri, hasa wasanii kwa wasanii wanapoonekana kusikiliza,
kutambua, na kukubali kazi zinazoendelea kwenye industry hii ya muziki
wetu.
|
No comments:
Post a Comment