![]() |
Inavyodaiwa Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili na hivyo alipewa camera aina ya Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo. Sasa waandaaji hao wanadai kuwa walimpatia Prof hela yake iliyokuwa imesalia.
Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka warudishiwe fedha yao.
Polisi wanashughulikia kesi hiyo na Prof aliyekuwa ameingia makubaliano ya show nyingine katika ukumbi wa Jamboree December 31 aliitosa show hiyo.source na gumzo la jiji |
No comments:
Post a Comment