![]() |
DNA |
Rapper DNA Kutoka Grandpa Records
Kenya Amesema hata kubali Chama chochote au Mwanasiasa nchini Kenya
Atumie wimbo wake wowote katika kampeni za Siasa bila ruhusa na
maelekezo maalum kutoka record lebel yake ya Grandpa. DNA ambaye
ameshawahi kuipeleke Banki fulani mahakamani kwa sababu za kubadilisha
wimbo wake wa Banjuka Ukawa Benkika amesema vyama vya siasa hupenda sana
kubadilisha au kutumia nyimbo za wasanii bila ruhusa zao. DNA
alikaririwa na sammisago.com akisema hajafunga milango kwa wale
wanaotaka kutumia Melody au wimbo wa Maswali ya Polisi kwenye kampeni
ila awe tayari kufata maelekezo na makubaliano ya Record lebel hio.
Pia
kuhusu vigezo vya chama ,DNA amesema chama atakacho kipa wimbo wake
lazima kiwe ni chama kilicho saidia vijana na wananchi wa Kenya. Hataki
wimbo wake uhusike kwenye chama kisicho tekeleza sera na ahadi zake.
No comments:
Post a Comment