Sunday, January 6, 2013

RAYUU ALALAMIKA KUCHAFULIWA NA AKAUNTI FAKE YA FACEBOOK ITUMIAYO PICHA YAKE



BAADA ya msanii wa filamu na tamthilia bongo Rayuu, kudaiwa kuwa anatumia mtandao wa kijamii wa facebook kuwaomba wanaume hela, ameamua kuweka wazi kuwa hausiki na ishu hizo na kudai kuwa kuna mmoja wa wasichana wanaotumia picha zake kwenye ukurasa wake akijifanya ni yeye ndiye anayehusika na ujinga huo kwani huwadanganya wanaume kuwa yeye ndiyo Rayuu wakati sio kweli.

Alisema kuwa aibu hiyo alianza kuipata kwenye msiba wa marehemu Sajuki, ambapo baadhi ya wanaume walioombwa fedha hizo walianza kumuuliza na kujikuta akiwa hana cha kuwajibu huku akishikwa na butwaa kuwa hajawahi kufanya tukio kama hilo.

“Baadhi ya wanaume wamekuja wakidai kuwa nilikuwa nawaomba hela kwenye mtandao wa facebook lakini baada ya kuzungumza nao sana wakanitajia jina la huyo dada na hata mimi simjui tena si rafiki yangu nashindwa kuelewa ni kwa nini anafanya hivyo,” alisema.




BAADHI YA STATUS ZA ASHA  AKIOMBA PESA



HII NDO AKAUNTI  ORIGINAL YA RAYUU 

No comments:

Post a Comment