UONGOZI wa Serikali ya
wanafunzi wa Chuo cha Usimamazi wa Fedha (IFMSO) cha jijini Dar es Salaam,
umesema hali ya usalama kwa sasa katika Hosteli za Kigamboni
inaridhisha.
Waziri Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema jana kuwa
tangu iundwe timu ya polisi inayoshirikiana na wanafunzi hao hali imekuwa tulivu
kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena katika
hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya ripoti ya timu hiyo
itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam,
Suleiman Kova.
“Kuna amani sana, misako
imefanyika lakini ripoti itatolewa Januari 30 na Kamanda Kova,”
alisema Sarungi.
Kauli ya Kiongozi huyo wa wanafunzi haikutofautina na
ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Englbert Kiondo, ambaye alisema taarifa
inayohusu hali ilivyo itatolewa na Kamanda Kova.
Kwa upande wa wakazi wa Kigamboni, walisema kuwa wameshuhudia polisi wakifanya doria maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kabla wanafunzi hawajaandamana.
Walisema pia wameona polisi wakiwakamata wahalifu
kwenye maeneo hayo kutokana na misako wanayoifanya hali ambayo imeleta utulivu
kwenye mji huo.
“Kwa sasa kumetulia
inawezekana wanasikilizia (wahalifu), likini ingetakiwa polisi wawakamate wale
vinara kwa sababu wanawafahamu” alisema Salum Rashid mkazi wa eneo
hilo.
Naye mkazi mwingine anayejishughulisha na biashara ya
kioski, alisema kuwa kumekuwa na utulivu kwani hata wanafunzi ambao ndiyo wateja
wake wakubwa wanamwambia kuwa wanaweza kuacha vitu wakavikuta
salama.
No comments:
Post a Comment