
MISS Temeke 2006/07 mwenye ‘taito’ kibao Bongo, Jokate Mwegelo
anadaiwa kuchumbiwa kwa siri nyumbani kwao, Songea mkoani Ruvuma
alipokwenda kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya, Ijumaa Wikienda
limenyetishiwA
Kwa mujibu wa sosi wa karibu wa staa huyo, Jokate alitimba Songea akiongozana na rafiki zake wawili pamoja na baadhi ya ndugu.
Chanzo hicho kilidai kuwa kilipochunguza amekwenda kufanya nini mkoani
humo, ndipo ikabainika kuwa alikwenda kusherehekea Mwaka Mpya
akiongozana na wazazi wake anaoishi nao Dar, lengo likiwa kukamilisha
mambo ya mila kwani alikuwa ameposwa na mchumba ambaye hakutajwa.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa nyumbani kwa akina Jokate ambaye aliapa
kuwa lazima mwaka huu aolewe, kulikuwa na wageni wengi ambao miongoni
mwao ndiyo waliopeleka posa.
Baada
ya habari hizi kutua mezani, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Jokate kwa
njia ya simu ambaye alikiri kwenda kwao Songea lakini hakutaka
kudadavua ishu ya kuchumbiwa.
“Mh! Watu ni wambeya jamani! Mimi
nilienda kwetu na ninatarajia kufanya kitu kikubwa huko Songea
mtakisikia ‘soon’,” alisema Jokate huku akicheka.
No comments:
Post a Comment