Wednesday, February 13, 2013

HATIMAYE MAMA LULU NA MAMA KANUMBA WAPATANISHWA


Hatimaye mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amepatanishwa na mama mzazi wa Lulu baada ya mlolongo mrefu na mgumu wa jitihada za kuwapatanisha kina mama hao wawili.

Chanzo chetu cha kuaminika  kimeripoti kwamba mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alikua mzito kupatanishwa kwa sababu ya kukasirishwa na kitendo cha mama mzazi wa Lulu ambae hakuwahi kufika msibani wala kutuma salamu za pole kwa mama Kanumba.

Baada ya Lulu kutoka kwa dhamana, mama mzazi wa marehemu Kanumba alisema yuko tayari kuonana na Lulu kwa sababu ni mtoto na hana tatizo nae lakini akasisitiza kama Lulu atakwenda kuonana nae ni sawa ila asiende na mama yake.

Wazazi hao wamepatanishwa jumapili february 10 2013 ambapo Lulu alikuepo kama muhusika mkuu wakati huo wa upatanisho, kwa siku zote mwigizaji huyu alikua akiomba kupatanishwa na mama wa Marehemu, pia alikua akisisitiza kuomba mama yake apatane na mama Kanumba,


Sababu za Mama Lulu kushindwa kwenda msibani alisema kwanza ni uoga kutokana pia na jinsi vyombo vya habari vilivyopamba, na nyingine ni machungu aliyokua nayo dhidi ya waigizaji hao wote wawili ambao alikua hajui kama walikua wapenzi, alikua anajua Marehemu anamfundisha Lulu usanii tu.

Mapatano yalisimamiwa na wazee wawili pamoja na watu wengine wa karibu wa familia na ilichukua dakika 240 kazi kumalizika kutokana na Mama mzazi wa Kanumba kuwa mgumu kiasi chake.

Baada ya kupatanishwa imeelezwa ndio mama mzazi wa Marehemu Kanumba, mama mzazi wa Lulu na watu wengine kadhaa wa karibu wa hizo familia, walikwenda kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba Kinondoni Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment