BAADA
ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina
la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na
changamoto za maisha.
Akizungumza na Maisha msanii wa filamu
ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu familia ya Lulu Mahfudh Hussein
'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule
ili aweze kuendelea na masomo yake
Alisema kuwa ingawa familia
ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani
familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake
anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo
Dkt.
Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo
hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu
kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele
"Hapo awali alikuwa na
uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa
anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa
akifanya mammbo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia"
alisema
Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari
kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha
hivyo jambo la msingi ni yeye kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani
umri wake bado ni mdogo na ananafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake
Akizungumzia
kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba
amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya
kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia
No comments:
Post a Comment