Sunday, December 30, 2012

DJ CHOKA ATOA MANENO MAKALI KWA WANAO MTUKANA KWA KUUZA WIMBO MPYA WA ROMA 2030

Naomba niseme hichi kitu... MIMI NI SHABIKI NAMBA MOJA WA WASANII WOTE TANZANIA NA KIKUBWA ZAIDI HASWA WALE WANAOFANYA VIZURI KWENYE GAME HILI LA BONGO. Juzi rafiki yangu na pia patna wangu kwenye business Roma Tongwe alitoa wimbo wake mpya 2030 na akaamua yeye kuja kivingine yaani ili uupate wimbo wake lazima uununue kwa shs elfu 3 na hakutaka uwepo kwenye site au blog zozote. Watu wengi walitarajia wimbo nitauweka kwenye blog kama nifanyavyo nyimbo za wasanii wengine, sasa sikuweza kufanya hivyo kutokana sikupewa ruksa na wamiliki wa wimbo huo badala yake nikawa naupromoti ili watu waweze kuununua kwa namba ambazo ni za ROMA mwenyewe na si namba zangu. Sasa wametokea watu wamenitukana sana na kusema wimbo nasikiliza mwenyewe getto na demu wangu bila kufahamu mimi mwenyewe rafiki mkubwa wa ROMA natakiwa niwe nao ni lazima niununue ili kumuunga mkono mshkaji wangu ili maisha yaendelee hata nikija na biashara yangu na yeye pia atanunua ndio urafiki ulivyo. Sasa nakushangaa wewe unaniita CHOKO kwanza ukiniita Choko naona kama umekosea herufi badala ya Choka ukaweka O so haliniumi coz nimezoea kuitwa hivyo na Haters so naona kama unanisifia tu. NATAMKA MANENO HAYA, NAHESHIMU KAZI YA MTU NA NAHESHIMU JASHO LA MTU NA NDIO MAANA SIWEZI KUFANYA KITU BILA RUKSA YA MTU, Mtoto mzuri ni yule aliyepata malezi bora kutoka kwa wazazi wake na akikuwa atanyooka na kuwa vile vile kama alivyolelewa na wazazi wake. NIMEMALIZA #Roma2030

No comments:

Post a Comment