Monday, December 31, 2012

FAHAMU KUHUSU CHAMELEONE KUVAMIWA NYUMBANI KWAKE.


Jose Chameleone
Msanii wa Uganda Jose Chameleone amenusurika kuuwawa baada ya mtu ambaye alikuwa na nia ya kumdhuru kwa kuvamia nyumba yake kujimwagia mafuta ya petroli na kujichoma moto baada ya kushtukiwa na mke wa Chameleone Daniella.Tukio hilo la kushtukiza lilitokea jana asubuhi baada ya mvamizi huyo Robert Kalamagi kuingia kwenye nyumba ya Chameleone wakati geti lake likiwa halina mlinzi, huku Chameleone akiwa ameuchapa usingizi baada ya kutoka kwenye shoo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Wilaya ya Kijjansi Ibrahim Saiga amesema polisi wanachunguza iwapo mtu huyo alikuwa ametumwa kumdhuru Chameleone ama alikuwa na nia ya kuiba tu

No comments:

Post a Comment