Sunday, December 30, 2012

ROMA AAMUA KUUZA WIMBO WAKE MPYA KWA SH. 3000 HUKU NIKKI WA PILI NAYE AKITUMIA M-PESA KUIUZA DVD YAKE

Wasanii wanazidi kuwaza kila siku jinsi ya kukwepa kuibiwa kazi zao ambazo ni jasho lao wanalotoa booth baada ya kusumbua akili zao na kufanyia kazi vyema mtaji wa kipaji walichopewa na Mungu.

Asilimia 90 ya wasanii wa Hip Hop hawapeleki kazi zao kwa wasambazaji bali huuza wenyewe ili kukwepa kuwafaidisha watu wengine kwa jasho lao.

Staili ya uuzaji iliyopewa jina la ‘kuuuza tapes kwenye bag’ inazidi kupatiwa mbadala kama sio kuboreshwa ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Roma mkatoliki ambae ametambulisha wimbo wake alioupa jina la ‘2030’, wimbo ambao unasubiriwa kwa huwa hadi sasa na fans wake kibao waweze kuupakua kwenye mtandao, sasa amekuja na staili tofauti ambapo anauuza wimbo huo kwa Tsh. 3000 tu .

Roma kupitia ukurasa wake wa facebook, ameelezea kuwa mteja wake atatuma pesa hiyo kwa njia ya simu pesa na email yake ama atatumiwa kwa njia ya Whasapp, kisha Roma atamtumia wimbo huo, lakini kwa makubaliano pia kuwa hatausambaza wala kuugawa ili kusapoti kazi yake iendane na kipato chake. 
 
Roma anasema kwa wale ambao hawana uwezo wa kununua basi watausikiliza tu redioni.

Nikki wa pili
Nikki wa Pili ambae ni msemaji wa WEUSI pia alizindua aina mpya ya usambazaji wa kazi za wasanii akianza na kazi yake, na hiyo December 23, katika tamasha la ‘Funga Mwaka la Weusi’ lilifanyika Dar-es-Salaam, Club Maisha, ambapo walizindua rasmi DVD ya Kum Kubam na wimbo mpya wa Lord Eyez “No More Drama”.

Katika aina hii mpya ya usambazaji, Mteja ama shabiki anatakiwa kutuma pesa kwa njia ya M-Pesa kiasi cha Tsh. 4,000 kisha atapewa CODE NUMBER ambayo ataipeleka kwa wakala wa Fichuka Dar na kupewa DVD hiyo ya BUM KUBAM. 
 
Siku moja baada ya tamasha hilo, WEUSI waliwatumia watanzania ujumbe ulioandikwa KUM KUBAM kama Attention kisha ukasomeka hivi;

“kupata CODE NUMBER ili ukachukue BUM KUBAM DVD kwa wakala wa Fichuka Dar, Lipa kwa MPESA,Namba ya kampuni 212121,Kumbukumbu Na. Malipo BUM KUBAM, kiasi 4,000.”

Kwa kweli sasa wasanii wanaonesha kuwa na muamko wa vitendo zaidi na kuutumia vizuri ulimwengu wa sayansi na technolojia, nice Move Roma na WEUSI, mwaka 2013 ukiongeza sapoti wasanii waliyoahidiwa na serikali najua tutafika mbali.

No comments:

Post a Comment