VENGU ANA THAMANI KUBWA KWANGU,SIWEZI KUMUACHA WALA KUMSARITI JAPO NI MGONJWA ''STELLA''
MISS
Kinondoni 2009, Stella Mbuge amefunguka kuwa ugonjwa wa mpenzi wake
Joseph Shamba ‘Vengu’, memba wa Orijino Komedi si sababu ya kumuacha na
kuhangaika na wanaume wengine. Akipiga stori na mpekuzi , Stella
alisema, anatambua kuugua ni sehemu ya maisha na jambo kubwa kwa sasa ni
kumuombea mpenzi wake huyo apone haraka na kuendelea na maisha yao kama
kawaida.
“Vengu
ana thamani kubwa kwangu, siwezi kumuacha wala kumsaliti. Ndugu zake
wananipenda na kunipa ushirikiano mzuri. Nashukuru anaendelea vizuri na
ninaamini siku si nyingi atarudi kazini,” alisema Stella.
No comments:
Post a Comment