MAMA mzazi
wa staa wa Bongo Fleva mwenye skendo ya kubwia madawa ya kulevya,
Rehema Chalamila ‘Ray C’, Magret Mtweve ametoa tamko kali dhidi ya
aliyekuwa mpenzi wa mwanae, Isaac Makuto ‘Lord Eyez’ kutotia mguu
nyumbani kwake Kunduchi, Dar.
Mama Ray C
alichimba mkwara huo wakati akizungumza na Mpekuzi wetu Jumatatu
iliyopita alipoulizwa kama Ray C amerudi nyumbani kwake baada ya
kutoweka kitambo.
“Amerudi
jana jioni (Jumapili). Nilipomuuliza amesema alikuwa Kariakoo, lakini
hataki kuwataja aliokuwa nao wala alichokuwa akikifanya.
“Nimekuwa
nikizunguka kwenye makanisa mbalimbali kumuombea njia, naona ameanza
kuleta matumaini lakini sitaki kabisa kumsikia mtu anayeitwa Lord Eyez,
yeye na wenzake ndiyo waliomsababishia matatizo haya mwanangu,” alisema
mama huyo.
No comments:
Post a Comment