Sunday, December 30, 2012

ZANZIBAR YAENDELEA NA MAANDALIZI YA KUHAMIA KATIKA MFUMO WA DIGITALI



 Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali juu ya suala zima la kuuingia katika mfumo wa Digitali huko katika ukumbi wa habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar
 Mwandishi wa habari Bw.Salum Vuai akiuliza suali kwa Waziri hayupo pichani juu ya upatikanaji wa vinga`muzi huko katika ukumbi wa habari maelezo mjini Zanzibar.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akijibu maswali ya waandishi wa habari hawapo pichani kulia ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Khamisi Hamadi
Jengo linalotarajiwa kufungwa vifaa vya mitambo ya Digitali lililopo Rahaleo mjini Zanzibar.
----------------------------------------------------------
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia yatazimwa rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28 mwakani ili kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.
Waziri wa habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya kuhamia katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.

Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu ambapo kwa zoni ya Zanzíbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe mwisho rasmi wa matangazo ya Analogi.
Waziri Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.

No comments:

Post a Comment