Mkurugenzi
wa Tiba wa Hospitali ya The Aga Khan, Jaffer Dharsee, amesema hali ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba
(pichani), sio nzuri na bado anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari
na wauguzi. Dk.
Dharsee alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa alikuwa na malaria
kali iliyosababisha kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na yuko
huko hadi sasa akiwa katika uangalizi wa katibu wa madaktari.
Msemaji
wa familia ya Manumba, James Kilaba, alisema hali ya ndugu yao inaleta
matumaini tofauti na ilivyokuwa awali na zaidi wanawasikiliza madaktari
kwa sababu ndio wanaojua hali yake.
Kilaba aliwaomba Watanzania kumuombea ndugu yao ili apone na kuendelea kutimiza wajibu wa kulitumikia Taifa.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwano Rais Jakaya Kikwete jana walifika hospitali hapo kumjilia hali Kamishna Manumba.
Wengine ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete; Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP), Saidi Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment