Thursday, January 24, 2013

BREAKING NEEEWZ!!! WANANCHI WAVAMIA NYUMBA ZA POLISI KIBITI WAZICHOMA MOTO


Kundi la wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilayani Rufiji na kufanya vurugu kubwa baada ya raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.

Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi, ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.

Habari zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanaendelea kuteketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya Polisi kuendelea kufanya juhudi za kuwatawanya kwa mabomu katika eneo hilo.

Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.

Hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu. Vurugu zinaendelea,

No comments:

Post a Comment