Saturday, January 26, 2013

CHANZO CHA VURUGU ZA JANA MASASI HIKI HAPA!



 






CHANZO cha vurugu za jana Mkoani Mtwara imeelezwa kuwa ni askari wa wanazinguka mjini na pikipiki maarufu kwa jina la Tigo kumkamata dereva wa pikipiki mmoja na kuanza kumpiga. Madereva hao walipoona tukio hilo la mwenzao kupigwa waliingilia kati mzozo huo na kumtoa mwenzao kwenye kadhia hiyo.
Baada ya kumtoa mwenzao kundi la madereva hao wa bodaboda waliandamana hadi kituo cha Polisi wilaya kwenda kueleza hisia zao lakini walipofika tu polisi walianza kufyatua mabomi yalio ibua hasira za wananchi na kuanza kusogelea ene la kituo hicho badala ya kukimbia.
Wananchi hao walijazana kwenye kituo hicho huku polisi wakiendelea kupiga mabomu lakini walionekana kushindwa wananchi haowakapata nguvu na kuanza kuchoma moto magari ya halmashauri na majengo.
Wakatoka hapo wakaenda kwenye nyumba ya Mbunge wa jimbo hilo wakaichoma moto wakaenda kwenye ofisi ya serikali ya mtaa, kwenye tawi la chama cha mapinduzi na baadaye kwenda kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa bodi ya Korosho Mama Anna Abdalla.
Kwamujibu wa mmoja wa wananchi wa Masasi aliyejitambulisha kwa jina la Mussa amesema ameona magari manne yakiwa na majeruhi wa tukio hilo wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Ndanda.
Aidha Mganga mmoja wa Hospitali ya Wilaya akizungumza na kituo kimoja Cha Radio alisema kuwa hospitalini hapo wamepokea miili ya watu watatu lakini amesema kuna uwezekano mkubwa idadi ya watu waliokufa ikawa kubwa zaidi kwasababu wapo wengine wamechukuliwa na nduguzao hukohuko kwenye matukio.

No comments:

Post a Comment