
Wengi wetu tumeingia katika mapenzi na wapenzi wenye tabia tofauti na baadhi wameshindwa kufahamu kama katika mapenzi hayo wanapata hasara au wananufaika. Sio kwamba katika mapenzi ni sehemu ya kuingia ukitazamia faida na manufaa tu, najua ziko nyakati za kujitoa kwaajili ya umpendaye lakini kwa wastani katika nyakati zote hizi wapenzi wote wawe na furaha mioyoni na hali ya kujisikia kutoshelezana katika maeneo yote ya maisha yao ya kilasiku na sio mmoja kujihisi kudhulumiwa, kutotendewa haki au kuegemewa zaidi kimahitaji.Nimekutana na lawama na malalamiko mengi sana kati ya wapenzi na hata maranyingine waliojikuta wameshaingia kwenye ndoa na nimeona nivema nitafute jinsi ya kuwasaidia wenye tatizo hili au kuku wezesha na wewe kumsaidia na mwingine.Wako wapenzi wanawake au wanaume ambao tabia yao nikutafuta namna ya kuzichimba pesa za mpenzi wake kwa namna yoyote ile. Mara nyingi wanaume wamekuwa wakiwalalamikia wanawake kuwa ndiyo wanaojifanya wanapenda kumbe wanachokitaka ni pesa au unafuu wa maisha kiuchumi kutoka kwa wapenzi wao wakiume. Lakini sikuhizi mambo yamekuwa na uwiano sawa, wako vijana wa kiume pia ambao kazi yao ni kuwalemea wapenzi wao kila siku kwa mahitaji yasiyoisha. Leo watasema wanashida hii, kesho shida nyingine itaibuka, na keshokutwa atakuja na jipya pia. Hali hii huyafanya mapenzi yakawa butu sana hatakama anayeelemewa hajaweza kusema kwa uwazi maumivu anayo yapata.

Huyu mpenzi wakike au wakiume mwenye tabia hizi huwa ndani ya moyo wake anajijua kabisa kuwa hana mapenzi ya dhati na shida yake ni kuyapunguza matatizo aliyo nayo, na maranyingine sio kwamba ana matatizo sana ila baada ya kuona mwanya wa kupata anachohitaji wakati wowote basi atatafuta hitaji lolote na kulipa umuhimu ili kukuonyesha uharaka wa kumsaidia. Kamwe haogopi wala kuhofia yeye tu kuonekana ndio mwenye shida kila siku na wala sio mpenzi mwingine, jiulize, iweje shida ziwe kwako kila siku tu?Wala huitaji kuwa tajiri sana ili wapenzi wa aina hii wakuvae, kama unampenzi wako wa kawaida tu an labda umeshawahi kujihisi kwamba mpenzi wako anaonyesha dalili za kuipenda hela yako zaidi, basi wewe tayari unanafasi kubwa ya kuwa mhanga wa wapenzi wa aina hii. Inabidi ujichunge na kuwa macho sana kwasababu wanapokupata huhakikisha wewe ndio unakuwa jawabu la maswali yao yote yanayohusu uchumi wao binafsi na maranyingine hata uchumi wa ndugu zake.

Iko tofauti kubwa kati ya mpenzi mpenda pesa zako na yule mpenzi ambaye unamsaidia na anauthamini msaada unaompa na kwamba hakufanya kusudi kulionyesha hitaji lake kwako ili umsaidie. Mpenzi mpenda pesa yako huhitaji chochote kutoka kwako na hata baada ya kukipata hauthamini msaada huo, maranyingine anaweza hata kukudhihaki kama yamkini umempa msaada chini ya kiwango alichotarajia kukipata kutoka kwako. Sio hivyo tu, mpenzi mpenda pesa zako anaweza kukuacha kimapenzi pale anapoona uwezowako wakumsaidia unapungua au kunamazingira ya uwezo huo kupungua huko mbeleni, mfano; anafahamu umeachishwa kazi, au umesimamishwa kazi, au umepata hasara kubwa katika biashara yako, au unapitia kipindi chochote kigumu kimaisha basi yeye badala ya kuumia au kusikitika na wewe atatafuta namna ya kukukwepa na kukuacha iliyeye akatafute mfadhili mwingine. Wapenzi wa jinsi hii kamwe hawapendi kusikia eti huna hela, wao hufurahia uharaka wa wewe kutatua matatizo yao tu.


No comments:
Post a Comment