Wanafunzi wakiwa na mabango leo mjini
dodoma.
ZAIDI ya wanafunzi 4000 wa Chuo Kikuu cha St. John’s
kilichopo mjini DODOMA wameandamana
wakililalamikia Jeshi la Polisi Nchini kwa kushindwa kuthibiti vitendo vya
matukio ya ubakaji na kulawitiwa yanayofanyika chuoni
hapo.
Wanafunzi hao ambao waliandamana umbali wa kilomita
tatu leo kutoka chuo kilipo na kuishia
viwanja vya Mwalimu Nyerere walidai wanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii
kutambua vitendo vya kikatili vinavyofanyika chuoni hapo.
Maandamano hayo
ambayo yalikuwa yakisindikizwa na
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, yalipita katika
mitaa mbalimbali ya Manispaa ya
Dodoma.
Waandamanaji hao ambao mbali na kuimba nyimbo za
kulilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa
kuthibiti vitendo hivyo, pia mabango waliyokuwa wamebeba yalikuwa yakililaumu jeshi
hilo.

Askari jeshi la polisi wakijariobu kuwazuia wanafunzi
leo mjini dodoma
No comments:
Post a Comment