
KATIKA hali isiyo ya kawaida, mastaa wa kike ndani ya Bongo Movies,
waligoma kuosha vyombo katika msiba wa Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Ijumaa
Wikienda lilishuhudia.
Mgomo
huo ulioleta tafsiri mbaya kwa mastaa wa kike, ulitokea Januari 4,
mwaka huu nyumbani kwa marehemu Tabata-Bima jijini Dar mara baada ya
taratibu za maziko kukamilika.Mama Abdul ambaye ni mwigizaji
mkongwe, aliwataka wasanii wa kike wainuke wakaoshe vyombo pasipo
kuhofia kuharibu kucha zao za kubandika lakini wachache walitii huku
wengi wao wakiendelea kung’ang’ania viti.
Mastaa ambao walionesha
kushiriki kazi mbalimbali msibani hapo siku hiyo ni Salome Ndumbagwe
Misayo ‘Thea’, Koleta Raymond ‘Coletha’, Suzan Lewis ‘Natasha’,
Yvone-Cherry ‘Monalisa’ na Jacqueline Wolper.
Sajuki alifariki dunia
Januari 2, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa
amelazwa kwa matatizo ya muda mrefu ya saratani ya ngozi, uvimbe tumboni
na upungufu wa damu.
No comments:
Post a Comment