Monday, January 7, 2013

HIKI NDIO KISA CHA WEMA KUSHINDWA KUHUDURIA MSIBA WA SAJUKI HIKI HAPA


Wema Isaac Sepetu.
KATIKA hali ya kushangaza, Wema Isaac Sepetu hakuonekana kwenye maziko ya staa mwenzake wa filamu za Kibongo, Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’, yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lililozua minong’ono kutoka kwa mashabiki wake na mastaa wenzake lilitokea Januari 4, mwaka huu ambapo watu walikuwa wakimuulizia Wema na kushangazwa kutoonekana kwake msibani.
“Wema siyo mtu wa kukosa kufika kwenye msiba wa staa mwenzake, angekuwepo ungemuona tu,” alisikika dada mmoja aliyeonekana kuwa na shauku ya kumuona Wema.
Duru za habari kutoka kwa watu wake karibu zilidai kuwa siku alipofariki Sajuki Wema hakufika msibani kwa sababu dada yake alijifungua.
Walidai kuwa kesho yake alisikika akisema ataenda msibani hapo lakini hadi siku Sajuki anazikwa Wema hakuonekana.
Habari za kina zilisheheresha kwamba siku ya maziko hayo Wema alidaiwa kuwa studio akirekodi ngoma yake mpya ambayo anatarajia kuiachia mwanzoni mwa mwaka huu, ili naye ajiweke poa katika gemu la muziki wa Kizazi Kipya, ishu ambayo ilithibitishwa na meneja wake, Martin Kadinda.

No comments:

Post a Comment