JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo
zitatoa wanafunzi 5,000 waliomaliza kidato cha sita watakaojiunga na
jeshi hilo.Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika
taarifa yake jana kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo
ifikapo Machi 2, mwaka huu.Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma,
Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule
nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa
Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos.Nyingine ni Ashira,
Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa
na Ruhuwiko-Songea.
No comments:
Post a Comment