Tuesday, January 22, 2013

HIZI NDO FOMU ZA KUJIUNGA NA BIG BROTHER AFRICA-2013 KWA WANAOTAKA


Msimu wa nane wa shindano la Big Brother Africa unatarajia kuanza mwezi May mwaka huu.Tayari vijana wanaovutiwa kujiunga na shindano hilo wana nafasi ya kujaribu bahati zao.

Mwaka huu nchi 14 zinashiriki ambapo nafasi ya Liberia inachukuliwa na Ethiopia sababu ni kuhakikisha kuwa nchi nyingi zinashiriki.Nchi zitakazoshiriki mwaka huu ni: Angola, Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.

Washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 21, raia wa nchi wanazotaka kuwakilisha na wawe na passport.Watayarishaji wanatafuta washiriki wanaongea kiingereza vizuri na wanaopenda shindano hilo, wacheshi na wavumilivu.

Fomu za kujiunga zinapatikana hapa BIGBROTHER AFRICA -2013 ambapo fomu zilizokuwa printed zitapatikana kwenye ofisi za MultiChoice katika nchi zinazoshiriki kuanzia February 1, 2013.

Mwaka huu shindano hilo litaanza Jumapili ya tarehe 26 May na kuchukua siku 91.

No comments:

Post a Comment