BAADA ya kuwepo kwa vingi viulizo juu ya Wema Sepetu na mwanamitindo
Martin Kadinda kwenda Afrika Kusini wawili tu, modo huyo wa kiume
amevunja ukimya na kusema kuwa, haina haja ya kushangaa kwani yeye ndiyo
kila kitu kwa msanii huyo.
.
Akizungumza kwa kujiamini hivi
karibuni, Kadinda alisema yeye kama meneja wa Wema, ana kila sababu ya
kuongozana naye kila anapokwenda kwani ndiye anayemchagulia nguo, viatu
hadi ‘setting’ ya nywele.
“Watu wamesemasema sana juu ya safari
yangu ya Sauzi na Wema…jamani mimi ni kila kitu kwa Wema kwani ni meneja
wake, napaswa kujua kila anachokifanya, hata linapokuja suala la mavazi
mimi ndiye ninayemchagulia ‘so’ watu wasihoji sana,” alisema Kadinda.
No comments:
Post a Comment