LIBERT MSUYA STAA WA FILAMU YA HOUSE BOY:" Haitosahaulika
kwa historia ya sanaa ya filmua Tanzania ni miaka miwili tu
tumeondokewa na wapiganaji wenzetu ambao tulikuwa bado tunawapenda na
kushirikiana nao kwa kila jambo kuhusu sanaa yetu.Lakini Mungu ameonesha
upendo zaidi kwao na amewatwa.Tunawatakia mapumziko mema ya milele
Ameen"
MZEE MAGALI:" Sasa
ni wakati wa kuyakabidhi maisha yetu kwa bwana hakika maisha yamekuwa
mafupi sana wanaondoka vijana wadogo ambao ni nguvu kazi ya taifa. Lakini kazi ya mungu haina makosa"
NISHA" Jamani
sijui ni nini? kweli binadamu tunapaswa kukesha katika maombi maana
miaka hii miwili wameondoka ndugu zetu mfululizo...Lakini kazi ya muumba
haina makosa tuwaombee wapumnziko mahali pema peponi kwa vile wao
wametangulia sisi tupo nyuma yao" Amina
WEMA SEPETU: "Kwa
kweli hadi inaogopesha licha ya kuwa sisi binadamu kufa ni lazima
lakini inaumiza kuona vijana wenzetu wanaondoka mapema,Upande mwingine
nafahamu kila kitu hupangwa na mungu hivyo kazi yake haina makosa jina
lake lihimidiwe Ameeen"
ELIYA DEVID MJATA:"Kazi ya Mungu haina makosa Sajuki tulimpenda sana ndio maana wasanii,watanzania tuliungana kufanya jitihada za kunusuru maisha yake kwa kujitolea kwa michango mbalimbali lakini mwisho wa siku baba Mungu hakupenda. Kapumnzike kwa amani mdogo wangu" Ameen
BAMBO:"Nilimfahamu
Sajuki tangu Kaole ambapo alikuwa msanii mwenye ndoto za mafanikio
lakini kutokana na mapenzi yake aliyetuumba ametutoka na kazi yake
imeisha hapo kiimani. Hivyo kazi imebaki kwetu sisi tulibaki hai tunajiandaaje na
safari? Bwana ametoa na sasa ametwaa jina lake lihimidiwe milele Ameen"
J.WOLPER:"Kwa
kweli kifo cha Sajuki kimetacha kwenye wakati mgumu sio kwenye familia
yake tu bali ni kwa sisi thote tulimpenda sana lakini mungu amempenda
zaini tumuombee aipumnzishe roho yake mahali pema peponi Ameen "
MANAIKI SANGa mwanamuziki na muigizaji:" Rest In Peace Bro tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda sana, thote tuko njia hiyo hiyo mbele yetu nyuma yako"
No comments:
Post a Comment