Kwa ufupi
ASEMA HERI AFUKUZWE KULIKO KUIONA
IKISAFIRISHWA, MWENYEKITI WA CCM NAYE APIGILIA MSUMARI, MREMA, MBATIA
WAWAUNGA MKONO, DC ATAKA ELIMU KWANZA
MBUNGE wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji na Mwenyekiti wa CCM
Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene wamepinga kauli ya Rais Jakaya
Kikwete kwamba wakazi wa Mkoa wa Mtwara hawapaswi kuzuia gesi kwenda Dar
es Salaam.
Juzi, katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais
Kikwete alipinga madai ya wakazi wa Mikoa ya Kusini kutaka gesi hiyo
isisafirishwe kwenda Dar es Salaam, akisema madai hayo hayakubaliki
popote.
“Rasilimali inayopatikana popote katika nchi hii
ni mali ya taifa zima na hutumika kwa manufaa ya taifa na katu si mali
ya watu wa pale ilipogundulika au pale shughuli inapofanyika,” alisema
Rais Kikwete.
Viongozi hao mbali na kuonyesha misimamo ya kuzuia
nishati hiyo hata kabla ya kauli hiyo ya Rais Kikwete, jana
walisisitiza kwa nyakati tofauti kwamba, wataendelea kuunga mkono
jitihada za wananchi kupinga usafirishwaji wake kwa kuwa hiyo ni haki
yao.
Murji alisema yupo tayari kuvuliwa ubunge kwa
kutetea masilahi ya Wanamtwara wanaopinga gesi hiyo inayovunwa katika
Kijiji cha Msimbati, mkoani Mtwara huku Chinkawene akisema msimamo wa
chama chake ni kuungana na wananchi kupinga gesi kupelekwa Dar es
Salaam.
Alisema Serikali inapaswa kujenga mitambo ya
kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam... “Tulipoona hali
inakuwa tete, niliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili nini
msimamo wa chama katika hili. Kamati ya Siasa wakasema hawawezi
kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama, hivyo nikaitisha kikao
cha Halmashauri Kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa.”
“Katika kikao hicho, wajumbe walipinga kwa nguvu
zote suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam.
Wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya Wanamtwara yatakapowekwa wazi na Serikali.”
Wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya Wanamtwara yatakapowekwa wazi na Serikali.”
Mwenyekiti huyo alisema kwa maana hiyo, msimamo
huo si wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho
vinavyowakilisha wanachama na kwamba historia ya Mikoa ya Kusini jinsi
ilivyonyimwa maendeleo ilitumiwa na wajumbe kujenga hoja hiyo.
“Wakati sisi hatuna umeme hakuna aliyefirikia
kutuunganisha kwenye gridi ya Taifa… Barabara ya kutoka Mtwara kwenda
Dar es Salaam miaka 51 ya Uhuru sasa, haijakamilika. Lakini bomba
wanataka kujenga kwa miezi 18. Hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya
wengine?” alihoji Chinkawene akinukuu kauli za wajumbe wa kikao hicho na
kuongeza:
“Walizungumza mambo mengi, suala la kung’olewa kwa
reli, kukatazwa kulima pamba, kuuawa kwa kilimo cha karanga na mkonge.
Haya yote wanadai yamesababisha mkoa uendelee kuwa maskini na kwamba
tumaini lao limebaki kwenye gesi. Wamesema wapo pamoja na wananchi.”
Murji kwa upande wake, alisema amekutana na umoja
wa vyama vya siasa vilivyoratibu maandamano ya kupinga suala hilo na
kuwapongeza kwa kazi nzuri akisema wananchi wana haki ya kutetea
rasilimali yao.
Alisema yeye si mbunge anayewakilisha mawazo yake bungeni, bali ya wananchi... “Hivyo ni bora niungane na wananchi wangu kutetea masilahi yao; liwalo na liwe.”
“Nawapongeza viongozi wa vyama vya siasa kwa
ujasiri na uthubutu wenu wa kutetea rasilimali hii (gesi)… Tusidharau
hata kidogo malalamiko ya wananchi…” alisema Murji huku akishangiliwa na
wajumbe na kuongeza:Alisema yeye si mbunge anayewakilisha mawazo yake bungeni, bali ya wananchi... “Hivyo ni bora niungane na wananchi wangu kutetea masilahi yao; liwalo na liwe.”
“Nipo pamoja nanyi na hata ikibidi nivue ubunge, nipo tayari kufanya hivyo kwa masilahi ya wananchi….”
No comments:
Post a Comment