Saturday, January 26, 2013

MSANII MATUMAINI WA KAOLE YU MAHUTUTI, ANAHITAJI MAOMBI YENU WATZ

MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Tumaini Martin Mwakibibi ‘Matumaini’ anadaiwa yu mahututi nchini Msumbiji ambako alikwenda kwa ajili ya kufanya shoo akiwa na mchekeshaji mwenzake, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’.
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Herieth Chumila ambaye pia ni msanii, alisema alipokea taarifa za kuumwa kwa Matumaini kutoka kwa mtoto wake aishiye nchini humo na kumwomba msaada wa haraka kwa kuwa msanii huyo yupo katika hali mbaya.
Herieth alisema kwa sasa msanii huyo hawezi hata kutembea na mahitaji muhimu ya kibinadamu anayamalizia kitandani.
“Nilipata bahati ya kuongea na Matumaini ingawa kwa shida sana, aliwaomba Watanzania tumsaidie ili arudi nyumbani. Alisema ni bora aje kufia huku kuliko nchi za watu,” alisema Herieth.
Akaongeza: “Kwa yule ambaye ataguswa kumchangia awasiliane na mimi kwa ajili ya mchango ambao utamfikia Matumaini kule Msumbiji.”

No comments:

Post a Comment