Saturday, January 26, 2013

BREAKING NEWS: HALI SI SHWARI MTWARA GARI LA POLISI LACHOMWA MOTO NA INASEMEKANA NYUMBA YA MH HAWA GHASIA YABOMOLEWA MUDA HUU

Mwandishi wa habari aumia katika vurugu za kgesi mtwara zinazoendela muda


Askari wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kutuliza fujo Mtwara kwa kile kilichoelezwa ni vurugu zinazoendelea za gesi

*************

VURUGU zinaendelea mjini Mtwara ambapo kwa sasa wananchi wamechoma moto vyoo vya mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya Nyumba ya Hawa Ghasia Waziri wa Tamisemi na Mohamed Sinani Mwenyekiti wa CCM mkoa zilizopo mtaa wa Sinani.

Wakiwa katika mahakama ya mwanzo Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka kituo kikuu cha mabasi na soko kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.

Baadhi ya barabara zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi……



........ endelea kufuatilia gfrankson blog tutakuletea picha zaidi za hali ilivyo huko ......

No comments:

Post a Comment