Thursday, January 3, 2013

MWILI WA SAJUKI WAHAMISHIWA MSIKITINI HUKU MAANDALIZI YA MAZISHI YAKIENDELEA


MWILI msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki juzi alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya Taifa, Muhimbili.

Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) uliopo Kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.

Msanii Issa Mussa “Cloud” aliiambia mpekuzi kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote za kesho kwenda na muda.

“Muhimbili process za kuchukua mwili ni ndefu na hata huduma zao za kuosha mwili wa marehemu ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa hospitalini hapo.

“Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili” alisema Cloud. 
 
Masjid Shadhully ndio msikiti atakaoswaliwa Sajuki ambapo mwili wake utachukuliwa msikitini hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata na baadae kurudishwa tena Masjid Shadhully kwa ajili ya kuswaliwa na kwenda kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za mchana.
 
MAANDALIZI  YA MSIBA

Wasanii wa filamu Mike Sangu (kushoto) Jacob Steven ‘JB’ (katikati) na Denes Sweya ‘Dino’ wakipanga mikakati msibani hapo.
Mke wa marehemu Sajuki, Wastara Juma ‘Stara’, aliyejifunika akifarijiwa na waombolezaji.

JB akimpa pole mama yake mzazi Sajuki
Stara akiwa katika maombolezo.
JBakijiweka tayari kwa shughuli za msibani.

Baba wa marehemu Sajuki, mzee Kilowoko, akimsikiliza JB.

MAANDALIZI ya kumzika msanii wa filamu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ yanaendelea nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.

Habari za kuaminika ni kwamba Sajuki atazikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo saa  mchana.

No comments:

Post a Comment