Wednesday, January 2, 2013

PICHA MBALI MBALI ZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MSIBA WA SAJUKI



Pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba akipata maelezo mafupi kutoka kwa Rais wa  Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba (wa pili kushoto) kuhusiana na mikakati na mipango mbalimbali ya mazishi ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki,nyumbani kwao Tabata Bima,jijini Dar.Aidha kwa taarifa rasmi kutoka kwa Simon Mwakifwamba ameeleza kuwa mazishi ya marehemu yatafanyika kwenye makaburi ya Kisutu siku ya Ijumaa mapema saa tano asubuhi.Kuli kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.
Rais wa  Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba kuhusiana na taratibu mbalimbali kuhusiana na msiba huo,huku baadhi ya wasanii wengine mahiri wa filamu wakisikiliza kwa makini.
 Mazungumzo mengine ya hapa na pale yakiendelea kufanyika kuhusiana taratibu nzima za msiba wa Sajuki,ulioko Tabata Bima,jijini Dar.

Rais wa  Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba,kushoto ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.
 Baadhi ya Wasanii wa wakijadiliana jambo.
 Dua ikiendelea kusomwa nyumbani kwa marehemu Sajuki.
 Baadhi ya Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wakongwe wa filamu wakiendelea kuwasili nyumbani kwa marehemu Sajuki mapema leo jioni. 
Watu mbalimbali wakiwe wenye simanzi kubwa wakijadiliana jambo   
  Watu mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye msiba wa marehemu Sajuki jioni ya leo maeneo ya Tabat Bima,jijini dar.
 Mdau mkubwa wa Filamu hapa nchini Saimon Simalenga akijaribu kutoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa marehemu Sajuki mapema leo jioni.
 Badhi ya Wadau na Wanahabari wakiwa wamekusanyika kwenye msiba huo.
Ruge Mutahaba akisalimiana na Mkurugenzi wa ASET,Asha Baraka,pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba pamoja na Simon Mwakifwamba.
 Wakifarijiana.
 Vikao vikiendelea
 Ruge Mutahaba akiwa ameongozana Mh January Makamba wakisalimiana na baadhi ya watu waliokuwa kwenye msiba,walipokuwa wakiwasili

Baadhi ya Wasanii wakibadilishana jambo

No comments:

Post a Comment