MKUU wa Mkoa wa Mtwara Joseph
Simbakalia amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli yake ya
Desemba 21, mwaka jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya
kupinga mpango wa kusafirisha gesi.
Mkuu huyo wa Mkoa alijikuta akiomba
radhi baada ya kubainika kwamba yeye ndiye aliyechochea vugu mkoani humo
kutokana na kauli zake kwa wananchi hao,katika mkutano huo ulioendeshwa na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba amesikitishwa na
kauli yake aliyowahi kuitoa kwa wanachi wa Mtwara.
“Kupitia hadhara hii nawaomba radhi
kwa kuwakwaza, nimesikitishwa kwa kauli yangu ambayo imepokewa kwa hisia kwamba
niliwadharau,” alisema Simbakalia na kuongeza:.
"Najua kauli yagu iliwaudhi
wengi hivyo naomba mnisamehe ndugu zangu na naomba tuungane katika jitihada za
kutatua suala hili, kwani serikali imebaini kwamba kuna kila sababu ya
wWananchi kusikilizwa na kupewa tarifa za mara kwa mara juu ya suala hili la
gesi"
No comments:
Post a Comment