Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika
zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure
Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana
akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.
Chanzo hicho kimesema Daz alionekana
maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki
wa muziki pamoja na wasanii wenzake.
Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia
mwandishi wetu jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni
mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye ni Kichaa na amekuwa mtu
wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu.
“Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa
Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa
mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia
tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila
watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema.
Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu
alimtafuta Afande Sele, ndipo alipothibitisha kutokea kwa tukio hilo
nakusema ameshampatia taarifa dada yake Daz wa Dar es salaam.
“Kweli hali ya Daz ni mbaya sana
nimejaribu kumuweka sawa lakini nimeshindwa labda wakamfanyie matambiko
ya kwao kwasababu baba na mama yake walifariki na walikuwa hawaelewani
labda kuna matatizo ya kifamilia.” alisema Afande.
No comments:
Post a Comment